Thursday, September 21, 2017
Home > Bunge > Mkuu Wa Wilaya Ya Kinondoni Ally Hapi Aagiza Polisi Kumkamata Mbunge Wa Kawe Halima Mdee.

Mkuu Wa Wilaya Ya Kinondoni Ally Hapi Aagiza Polisi Kumkamata Mbunge Wa Kawe Halima Mdee.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumuweka ndani Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA, Halima Mdee akituhumiwa kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, DC Ally Hapi amesema kuwa mbunge huyo amemtukana Rais Dkt John Pombe Magufuli hivyo kulitaka Jeshi la Polisi limuweke ndani kwa saa 48 (siku mbili).

Hapi alisema kuwa mbunge huyo alimkashifu Rais Dkt Magufuli alipoongea na waandishi wa habari jana ambapo ametaka akamatwe, awekwe ndani kwa saa 48, ahojiwe na pia afikishwe katika vyombo vya sheria.

Mdee anatuhumiwa kutenda kosa hilo jana alipokuwa akizungumza katika Baraza ka Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) ambapo miongoni mwa mambo mengi waliyozungumzia ni kuhusu mimba kwa wanafunzi waliopo shule.

Haikuwekwa wazi ni tusi gani ambalo Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa BAWACHA alimtukana Rais lakini aliwataka viongozi wa halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA, kuwaruhusu watoto kuendelea na masomo baada ya kujifungua, mpango ambao Rais Magufuli alishaukataa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *