Thursday, September 21, 2017
Home > Featured_Slider > Shirika La Hali Ya Hewa Duniani Laja Na Mpango Wa Kuunusuru Mlima Wa Kilimanjaro Tanzania.

Shirika La Hali Ya Hewa Duniani Laja Na Mpango Wa Kuunusuru Mlima Wa Kilimanjaro Tanzania.

Shirika la Hali ya Hewa duniani (WMO), limekubali kuuingiza Mlima wa Kilimanjaro iliyopo Tanzania kwenye Program yake inayoshughulika na nchi zenye barafu ulimwenguni ili kuunusuru na janga la kuyeyuka kwa barafu .

 

Akizungumza na Wataalamu wa shirika hilo waliokutana jana jijini Arusha Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini, Dkt. Agness Kijazi amesema hiyo ni hatua ya msingi itakayotoa fursa kwa wataalamu wa hali ya hewa kufanya tafiti mbalimbali ili kubaini chanzo cha kupungua kwa barafu ya mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.

 

Kwa upande mwingine Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hatua hiyo pia itakuwa fursa kwa wataalamu kufanya utafiti kwenye maeneo mengine yenye barafu nchini Tanzania.

 

Nchi nyingine ya ukanda wa Afrika Mashariki inayotajwa kuwa na eneo lenye barafu ni nchi ya Kenya kupitia mlima Kenya.

 

Chanzo:ITV

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *