Thursday, September 21, 2017
Home > CCM > UVCCM: Ni Heri Serikali Ikose Mapato Kuliko Kuendelea Kunyonywa.

UVCCM: Ni Heri Serikali Ikose Mapato Kuliko Kuendelea Kunyonywa.

Na Mwandishi wetu Dodoma
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa hatua anazozichukua dhidi ya wabadhilifu Mali za umma kwani wamepelekea Taifa kuingia katika hasara kubwa.

UVCCM imesema kuwa watanzania wanapaswa kutanguliza mbele maslahi ya umma bila kujali itikadi za kisiasa, Makabila, Ukanda, Dini na Jinsia ili Taifa liweze kusonga mbele.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kikundi Cha Friends Of CCM, kundi ambalo dhima yake kubwa ni kuandaa miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika Kilimo na ufugaji ambayo itasaidia kutengeneza ajira kwa vijana.

Alisema Rais Magufuli ameanzisha Vita ya Kiuchumi dhidi ya mafisadi wa ndani na nje ya Nchi katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya Madini yote hayo amekusudia kuwanufaisha watanzania kupitia Rasilimali zao.

Shaka alisema Nchi inapaswa kuwa mstari wa mbele kumpongeza Rais na kumtia moyo kutokana na jitihada kubwa anazozifanya kuhakikisha analinda Rasilimali ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikipotea kutokana na uwepo wa watendaji wasiokuwa na uzalendo kwa ushirikiano mkubwa na baadhi ya mafisadi kuhujumu uchumi.

Alisema Kila mwananchi anahitaji kupata maendeleo na Maendeleo hayawezi kuja endapo kukiwepo na ufisadi ambao kwa wakati wote umekuwa sio Bora kwa mustakali wa uhai wa nchi.

Alisema watanzania wanapaswa kuachana na tabia ya kutumiwa na wapinga maendeleo ya Taifa Kwa kivuli Cha mfumo wa vyama vingi kwa kushirikiana na vibaraka ambao kazi yao ni kupinga kila kitu Cha maendeleo.

Aliwasihi wanachama wa kikundi hicho Cha Friends Of CCM kuwa maendeleo katika Taifa lolote huchagizwa na nguvu kazi za Vijana kwa ushirikiano na Wazee kwani ni rahisi kuvuka mtumbwi kwa sababu ya busara za Wazee.

Akisoma risala iliyoandaliwa na kikundi hicho mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti mwenza wa Kundi hilo la Friends Of CCM Bi Caroline Castor Malekela alisema kuwa katika kipindi Cha miaka ya 1990 Hadi Sasa kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya viongozi kuwa na tamaa ya kupora na kujilimbikizia Mali nyingi kwa manufaa yao binafsi.

Alisema kufanya hivyo ni ukosefu wa Maadili na kutokuwa na uzalendo hivyo kundi la mtandao la Friends Of CCM limekusudia kulivalia njuga tatizo hilo kutoa elimu ya uraia Mwema kwa kushirikiana na viongozi wa Chama na serikali.

Aliongeza kuwa CCM ni Chama pekee barani Afrika ambacho kinasimamia misingi ya haki, usawa, ulinzi, na usalama wa wananchi wake hususani katika Jambo la kipekee kabisa la kukabidhiana madaraka kwa muda mwafaka bila kukiuka katiba ya Nchi na ya Chama kwa hali ya Amani na usalama.
MWISHO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *